Katika picha ni wajumbe waliohudhuria katika kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa mwongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la utekelezaji,kikao ambacho kimehudhuriwa na wajumbe kutoka Halmashauri ya Mji Makambako na TASAF makao makuu.
Akizungumza na hadhara katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Makambako,Mkurugenzi mtendaji wa TASAF, Ladislaus Joseph Mwamanga amesema kupitia mradi wa TASAF kiujumla toka mradi huo umeanza yapo mabadiliko mengi katika jamii kwa Tanzania bara na Zanzibar kwani wengi wa wamekuza uchumi katika familia zao kutokana na kuwezesha fedha ambazo zinatumika katika uzalishaji kwenye familia zao,TASAF imejitahidi kupunguza umaskini kwa kaya lengwa hasa kaya ambazo zilikuwa na hali ngumu ya uchumi na zile ambazo zilikuwa hazina uwezo wa kufanya kazi kutokana na uzee,ulemavu na hali duni ya kimaisha kwa ujumla,wameweza kufikiwa na huduma kama vila Afya,Maji,Elimu na mbiundo mbinu ya barabara katika maeneo yao na kazi inaendelea kwaajili ya kuwapata walengwa wenye sifa za kuwa wanufaika na mfuko huu wa TASAF.
Aidha wakati wa kikao hicho Zacharia Ngoma ambaye ni afisa msimamizi na ufuatiliaji TASAF makao makuu ametoa elimu juu ya kipindi cha pili awamu ya tatu ya TASAF kuwa ni uhakiki mkubwa kwaajili ya kuwaondoa wasio nasifa na kupata wale wenye sifa za kuwa walengwa na kujilidhisha kwa idadi ya walengwa wenye sifa ndio lengo kubwa ,kuwezesha kaya kuongeza kipato ,kuwezesha kaya kuongeza rasilimali zalishi na kuongeza uchumi ,kuwekeza katika watoto ili kuleta matokeo chanya yatakayodumu kwa muda mrefu,kuwezesha upatikanaji wa huduma za maji,elimu, afya na kukuza uchumi katika eneo husika.
Vile vile suala la utambuzi wa uandikishaji wa kaya za walengwa kua utafanyika mara baada ya mafunzo yatakayotolewa kwa wawezeshaji wa ngazi ya Halmashauri na kata ambao utafanyika kwa awamu hadi kukamilisha maeneo yote ambayo hayakufikiwa na utambuzi huo lakini pia zoezi hilo litashirikisha jamii yote na viongozi wa eneo husika kwa ujumla.
Aidha Afisa ufuatiliaji amefafanua kuwa katika suala la ruzuku kwa walengwa masharti ni muhimu sana kuyafuata hususani suala la watoto chini ya miaka miwili wanatakiwa kuhudhuria clinik mara moja kwa mwezi ,Wanafunzi kuanzia miaka sita hadi kumi na tano wanatakiwa kuhudhuri masomo sio chini ya asilimia themanini ya muda wa shule na mwakilishi wa kaya atatakiwa kuhudhuria warsha za jamiii kila baada ya miezi miwili kinyume na hapo malipo ya kaya husika yanaweza kusitishwa.
Kikao hicho kimeenda sambamba na maswali ambapo wajumbe wameuliza maswali kwa lengo la kupata ufafanuzi zaidi nakujenga uelewa. Miongoni mwa maswali ambayo yameulizwa ni pamoja na:Kama lengo la TASAF ni kuwafikia walengwa je endapo mlengwa alikuwa ni mlemavu hapo awali na akapona utaratibi unakuwaje?, Na kama mlengwa wa TASAF endapo inatokea anafariki fedha zake zinaenda wapi?,Mfumo wa kugawa fedha kwa walengwa kwa sasa ni wa njia ya kielectroniki je? suala la kupanda kwa makato ya miamala ya fedha haliwezi kuathiri malipo hayo?,Suala la udumavu katika mkoa wa Njombe bado ni kilio kikubwa je TASAF inawasaidiaje walengwa kuendelea kupambana na janga la udumavu katika jamii ambazo walengwa wanaishi ?.
Akijibu maswali ya wajumbe Mkurugenzi mtendaji TASAF amesema ;Endapo mlengwa wa mfuko wa TASAF alikuwa na tatizo la ulemavu na ikatokea akapona kwa namna moja ama nyingine basi atakuwa hana sifa ya kuwa mlengwa wa mfuko huo,Kuhusu mlengwa kufariki dunia mara inapotokea hivyo basa fedha ambazo ilitakiwa apewe mlengwa huyo zinarudi makao makuu ya TASAF kwaajili ya matumizi mengine kwakuwa mhusika tayari hayupo,Katika suala la makato ya simu ni kuwa gharama zote za malipo kwa njia ya mtandao au kielectronic ni jukumu la taasisi kwahiyo walengwa watapata fedha zao kamili kwakuwa taasisi Inabeba gharama hizo, Akimaliza majibu ya mchango wa TASAF katika kupambana na UDUMAVU amesema elimu inaendelea kutolewa kwa walengwa namna ya kuzuia udumavu katika familia zao hasa masuala ya lishe bora ya kila siku katika familia zao.
Kwa upande wa kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Makambako, Appia Mayemba amegusia suala uwepo wa TASAF kuwa umesaidia familia nyingi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako hasa katika suala zima la Afya ,Elimu na miundo mbinu kwa ujumla hivyo anaimani kuwa hata katika kupindi cha awamu ya Tatu ya TASAF ana imani kubwa kazi Itaendelea kuwafikia walengwa wenye sifa jambo ambalo litaleta matokeo chanya katika jamii.
Akifunga kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Hanana Mfikwa ameshukuru uongozi mzima wa TASAF kwa jinsi wanavyosaidia kaya zenye sifa za kuwa walengwa wa mfuko wa TASAF ili kufikiwa na mfuko huo na kupitia semina mbalimbali za TASAF zitawajenga watendaji na walengwa kwa kuzitumia vizuri fedha hizo ili fedha zinazo patikana ziwe endelevu katika kukuza uchumi katika jamii kwa ujumla,Kazi iendele.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa