Na. Lina Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi taasisi ya Taifa letu,Kesho yetu (TK movement) inayojishughulisha na kuhamasisha jamii hususani vijana kufanya mapinduzi ya kifikra na uchumi nchini ili kujenga Taifa lao la kesho.
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Johnson Mkoani Njombe, Mhe. Mtaka amesema kuwa, kwa sasa vijana wengi hawana mitazamo ya mbele kimaisha, kwa kutokuwa na matamanio yoyote katika kuzitumia fursa zilizopo,hivyo TK Movement ione namna ya kuwasaidia vijana kutengeneza kizazi bora kwa walio ajiriwa na walio jiajiri.
Mhe. Mtaka amewataka viongozi wa taasisi hiyo kushikamana katika kusimamia na kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo,ili kuleta mabadiliko kwa vijana kwa kuwabadilisha namna ya kufikiri ili wazione fursa na kuzitumia ipasavyo.
“Tutapofika hapo tunaweza kupata vijana wanaosema wanamshukuru sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Njombe,kwa sababu nilipeleka wazo langu la mradi kwenye asilimia 10 nikapewa mil 5,nimeweza kufanya biashara hii na nimezalisha hii na vijana wakaanza kujua na kujifunza badala ya kulishana ujinga mitandaoni” alisema Mhe. Mtaka.
Ametoa wito kwa vijana kutumia mitandao kwa manufaa kwa kuanza kuzingatia mambo yenye tija kama mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na mikopo ya asilimia 9 kwa wakulima,wavuvi na wafugaji, kwa kuzingatia mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa