Na. Lina Sanga
Tamko hilo lilitolewa jana na Mhe. Imani Fute,diwani wa Kata ya Kitandililo na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,katika Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2024 ngazi ya Halmashauri.
Mhe. Fute alisema kuwa ,kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 imekuja kwa wakati,na jamii inapaswa kuwekeza kwa wanawake ili kufikia maendeleo.
Aliongeza kuwa, katika nyaja zote za maisha ikiwa ni pamoja na nyanja ya jamii,wanawake wamekuwa chachu katika maendeleo ya jamii na malezi,nyanja ya afya ambayo bila mama kuwa na Afya njema hata watoto wake hawatakuwa na Afya nzuri.
Alibainisha kuwa,katika nyanja ya kiuchumi wanawake wamekuwa chachu muhimu ya ukuaji wa Uchumi,kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali hivyo wanaume na jamii hawana budi kuwekeza kikamilifu kwa wanawake kwani wao ndiyo wanaoleta rasilimali muhimu.
Alitoa wito kwa wanawake kutojisahau katika harakati za ukombozi wa mwanamke,bali wanapaswa kutambua utamaduni kwani wajibu wa malezi ni wao,na wanaume wanapaswa kutambua changamoto zinazowakabili wanawake kwani mwanamke si chombo cha malezi pekee bali wawapewe fursa mbalimbali za kiuchumi ili kukuza pato la familia na Taifa kwa ujumla.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni "Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa jamii".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa