Na. Lina Sanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Mapato ya Halmashauri ya Mji Makambako (Task force), Carlos Mhenga ametoa wito kwa Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji kusimamia na kukusanya mapato katika maeneo yao ya kazi kwa maendeleo ya Halmashauri.
Mhenga ametoa rai hiyo alipokua akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mapato ya Halmashauri pamoja na Watendaji Kata,Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Makambako katika kikao kazi cha ukusanyaji mapato,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri leo.
Ajenda kuu za kikao hicho ni namna ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kujadili changamoto mbalimbali za zoezi la ukusanyaji Mapato na kuzitafutia ufumbuzi,kwa maslahi ya walipaji(Wananchi) na Mkusanyaji(Serikali!), hususani katika chanzo cha ada ya taka na malipo ya vibali vya Ujenzi.
Amesema kuwa baadhi ya wananchi wanafanya ujenzi bila kibali cha ujenzi ambapo ni kinyume cha utaratibu,hivyo kila Mtendaji katika mtaa wake ahakikishe hakuna ujenzi holela na wananchi wapewe elimu juu ya umuhimu wa kibali cha ujenzi,timu ya mapato ipo tayari kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na ipo tayari kuhakikisha kila Mjenzi anapata kibali kwa wakati ili kuondoa ujenzi holela.
Mhenga,amesema kuwa mapato yanayokusanywa ndiyo yanayotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo za Halmashauri kama ujenzi wa madarasa,zahanati na vituo vya afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu.
Ametoa wito kwa wananchi wote kuhakikisha wanafuata taratibu za ujenzi kwa kulipia vibali vya ujenzi lakini pia kulipa ushuru wa Halmashauri kama ada ya taka ili kutunza Mji katika hali ya usafi,Kulipia leseni za biashara,kibali cha matangazo na sherehe,ushuru wa mazao ya chakula na misitu,kodi ya huduma,ushuru wa Madini na kuchangia shughuli za maendeleo katika Kata,Mitaa na Vijiji.
#LipakodinaushuruwaHalmashaurikwamaendeleoyaMjiwaMakambako
#Makambakompyainajengwanasisiwenyewe
#Jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa