Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mhe. Imani Fute katika mkutano ea uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha lishe na mpango ea kupunguza udumavu,katika Halmashauri ya Mji Makambako ikiwa ni kampeni ya Mkoa wa Njombe kutokomeza udumavu.
Mhe. Fute amesema kuwa, ipo haja ya wananchi kutambua lishe si jambo geni au ulaji wa vyakula vya aina fulani tofauti na vyakula vinavyopatikana kwenye maeneo yao.
Amesema kuwa, lishe inajumuisha ulaji wa vyakula vyenye virutubisho mbalimbali ambavyo vinapatikana kwenye maeneo mbalimbali, katika Halmashauri ya Mji Makambako kama vile viazi, mahindi, mayai, maziwa, mboga za majani pamoja na matunda.
"Niwasihi wazazi kuendelea kuwalisha vyakula vyenye virutubisho watoto wenu ili kutokomeza udumavu kwani vyakula vyenye lishe ni hivi hivi vilivyopo kwenye maeneo yetu, viazi, mahindi na hata vyakula vya kibena mang'eng'e na madinyu,lakini pia nyama hata simbilisi ni nyama tuache kutafsiri lishe kwa namna tofauti",alisema Mhe. Fute.
Ametoa wito kwa wanaume kushirikiana na wake zao kipindi cha ujauzito ikiwa ni pamoja na kumsindikiza kliniki na kumsaidia majukumu mbalimbali hadi atakapojifungua na kumaliza kipindi cha unyonyeshaji.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa