Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mwl. Fadhili Msilu akimwakilisha katibu tawala sehemu ya elimu na ufundi katika maadhimisho ya wiki ya elimu jumuishi,katika shule ya msingi Kahawa iliyopo Kata ya Kitisi katika Halmashauri ya Mji Makambako.

Mwl. Msilu amesema kuwa,lengo kuu la Serikali kuanzisha elimu jumuishi kwenye shule zote ni kutoa nafasi kwa watoto wote wenye mahitaji maalum kusoma shule yoyote pasipo kujali ulemavu alionao, kwa kuweka msingi wa usawa na kuondoka vikwazo vinavyoweza kuwazuia kuhudhuria masomo kama umbali,kupunguza unyanyapaa na kuchochea vipaji na ubunifu.
"Pokeeni wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanapofika shuleni kwenu hata kama anaonekana ana changamoto kubwa,mshirikishe Afisa elimu maalum ngazi ya Halmashauri ili atoe ushauri wa namna ya kumsaidia mtoto kwani kwa sasa shule zote zinatoa elimu jumuishi",alisema Mwl. Msilu.

Ametoa wito kwa walimu wakuu kuwapokea watoto wenye mahitaji maalumu wanaofika katika shule zao kwa kushirikiana na Afisa elimu maalum, ili kumsaidia mwanafunzi endapo ana changamoto kubwa badala ya kukataa kumpokea.

Naye, Bw. Romanus Mlimira, Afisa uthibiti ubora wa shule Halmashauri ya Mji Makambako ametoa wito kwa wazazi kushiriki kwenye maadhimisho ya wiki la elimu jumuishi, ili kushuhudia vipaji na uwezo wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya wiki la elimu jumuishi kwa mwaka huu inasema "Akili Mnemba,Nguvu ya Teknolojia wezeshi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum; Kuimarisha elimu jumuishi ,tuwape kipaumbele makundi maalum katika upigaji kura Oktoba 29,2025".

Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa