Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa leo na Mbunge wa jimbo la Makambako,Mhe. Deo Kasenyenda Sanga katika Mtaa wa Lupila wakati akihutubia wananchi wa Mitaa ya Lupila,Kisingile na Kitisi ikiwa ni sehemu ya ziara ya Mbunge katika Mitaa na Vijiji ndani ya jimbo la Makambako.
Mhe. Sanga amesema kuwa,ipo haja ya wananchi kuambiwa ukweli kwani Mitaa katika Kata ya Kitisi,barabara hazipitiki wala hazifanyiwi matengenezo mara kwa mara kutokana na ujenzi holela katika Kata hiyo na Serikali inatengeneza barabara sehemu zinazopitika.
Sikitu Pella,Mhandisi wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Makambako,amesema kuwa nyumba nyingi za Mitaa katika Kata ya Kitisi zimesogea barabarani na kuwa kikwazo cha kupitisha mitambo mizito kwa ajili ya matengenezo kwani hata ikipitishwa inaweza kusababisha nyufa kwenye nyumba na wananchi wataanza kudai fidia,hivyo kwa sasa wananchi wawe tayari kukubaliana na matokeo endapo nyumba zao zitapata athari wakati mitambo ikipitishwa wasidai fidia.
Moja kati ya barabara katika Mtaa wa Lupila
Ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Kitisi na Kata zingine kuhakikisha barabara zinapitika kwa kutojenga kiholela bila kufata mpangalio,ili zifanyiwe matengenezo kwa kadri fedha zinavyopatikana.
Pia, ametoa rai kwa wananchi kutunza miundombinu inayotengenezwa, hususani mifereji inayosaidia kupunguza maji barabarani kutokana na miteremko mikali kwani kuziba mifereji kunasababisha maji kukata barabara.
Katika mwaka wa fedha 2023/2024 TARURA itafanya matengenezo ya kawaida katika baadhi ya barabara katika Mitaa ya Kata ya Kitisi ikiwa ni pamoja na barabara ya Kambo -Kahawa,Mwembetogwa -Ngwale,Soko la mbao -Goligotha,Soko la Kimataifa ,Mwendamseke- Goligotha,Kitisi Makaburini-Kigala na ujenzi wa daraja linalounganisha barabara ya DS na A one Lodge.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa