Na. Lina Sanga
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Azimio ,Mwl. Maisha Mhapa wakati akiwasilisha taarifa ya wanafunzi walioripoti shuleni hapo baada ya shule kufungua rasmi leo kwa ajili ya kuanza mwaka mpya wa masomo 2024.
Mwl. Mhapa amesema kuwa,shule ya Azimio imevuka lengo la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza mwaka huu,na kusababisha ongezeko la wanafunzi kwa asilimia 4 tofauti na idadi kwa mwaka 2023.
Amebainisha kuwa, maoteo ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali kwa mwaka 2024 ilikuwa wanafunzi 19,wasichana 10 na wavulana 9 na hadi leo jumla ya wanafunzi 56 wameandikishwa kuanza darasa la awali wasichana 32 na wavulana 24 sawa na asilimia 294.5 ya lengo.
Aidha ameongeza kuwa, maoteo ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa mwaka 2024 ilikuwa ni wanafunzi 121,wavulana 58 na wasichana 63 na hadi leo jumla ya wanafunzi 131 wameandikishwa kuanza darasa la kwanza katika shule hiyo wasichana 69 na wavulana 62 sawa na asilimia 108 ya lengo.
Amesema kuwa, ongezeko hilo la wanafunzi limetokana na elimu bila malipo,kuondolewa kwa michango isiyo ya lazima pamoja na ujenzi wa miundombinu mipya ya shule hiyo, kupitia mradi wa BOOST kwani kupitia wazazi wengi wamehamasika kuwaandikisha watoto katika shule hiyo,tofauti na miaka iliyopita,kutokana na uchakavu wa miundombinu.
Ametoa wito kwa wazazi na jamii kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule ,wanaandikishwa ikiwa ni pamoja na watoto wenye ulemavu kwani wana haki ya kupata elimu.
Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha zilizotekeleza ujenzi wa shule mpya ya Azimio.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa