Katika picha ni kamati ya siasa ya wilaya ya Njombe wakiwa katika zoezi zima la ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa Halmashauri ya Mji wa Makambako ,kamati ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya Siasa Wilaya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe Bwana Edward Mgaya na timu nzima ya kamati ya Siasa ya Wilaya ya Njombe.
Miongoni mwa miradi ambayo imekaguliwa na kamati ya siasa Wilaya ni pamoja na Jengo lenye vyumba vya Madarasa Mawili katika Shule ya Msingi Magegele na Matundu kumi na mbili ya vyoo ambayo yanaendelea kujengwa kwa gharama ya shilingi Milion Hamsini na tatu(53,000,000) fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mradi mwingine ni katika shule ya Sekondari Deo Sanga ambapo vyumba vya Madarasa viwili vinaendelea kujengwa pamoja na Maabara ya somo la Kemia ili tu kuongeza tija ya ufaulu wa Wanafunzi hasa katika masomo ya sayansi kwa ujumla wake ,vyote hivyo vimegharimu tasrimu fedha za kitanzia shilingi Milion sabini (70,000,000) na zote zimetolewa na Serikali.
Ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kipagamo pia umetembelewa na kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe ambapo jengo hilo linajengwa kwa nguvu za wanaNchi na Halmshauri ya Mji wa Makambako.
Kamati ya siasa Wilaya pia imetembelea mradi wa Zahanati ya Nyamande iiyopo kata ya Kitandililo na kuona mafundi wakiendelea na ujenzi wa zahanati hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwasaidia wanaNchi kupata huduma mapema huku kamati ya siasa ikiridhishwa na kasi ya ujenzi wa zahanati hiyo,katika ujenzi huo takribani fedha za kitanzania Shilingi Milion Hamsini (50,000,000) zinaendelea kutumika katika ujenzi huo.Wakati huo zoezi la kukagua wodi katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Makambako yenye hadhi ya wilaya iliyopo Mlowa nayo imetizamwa na kamati ya Siasa wilaya ambapo takribani wodi mbili zinaendelea kujengwa katika Hospitali hiyo kwa gharama za Serikali na takribani Shilingi Bilion ishirini na tatu zimetolewa na Serikali kwa ujenzi huo yote haya ni lengo la serikali ni kuweka sekta ya afya katika Mandhari yenye weledi mkubwa na makini.
Akihitimsha tadhimini ya zoezi la ukaguzi wa miradi hiyo Mwenyekiti wa kamati ya siasa wilaya ya Njombe Bwana Edward Mgaya na timu nzima ya kamati ya Siasa Wilaya kwapamoja wamesema hali ya utekelezaji wa miradi ya Halmashauri ya Mji wa Makambako ni kubwa na inaridhisha kwa kuwa ubora wa majengo yaliyopo yanaendana na dhamani ya pesa inayotolewa hivyo ni vema matumizi ya fedha hizo yakawa mazuri na makini ili kuepuka dosari pindi majengo hayo yanapogauliwa mara baada ya kumalizika ujenzi wake, Lakini pia jambo la kutunza majengo hayo ili yaweze kutumika na hapo baadae limesisitizwa sana na kamati hiyo maana yake utangulizwe UZALENDO katika miradi hiyo ili itufae na hapo baadae.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa