Pichani ni Dk Ashantu Kachwamba Kijaji ambaye ameteuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari akichukua nafasi ya Dk, Faustine Ndugulile ambaye uteuzi wake umetenguliwa wakati huo Mheshimiwa Rais ameihamishia idara ya Habari katika Wizara hiyo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo.
Katika historia ya Dk Ashantu Kijaji Kielimu ni pamoja na: Elimu ya Msingi alisoma Kondoa katika shule ya msingi Kalamba kati ya Mwaka 1984-1990 akijiunga na shule ya Sekondari ya wasichana Kilakala iliyopo Mkoani Morogoro kati ya Mwaka 1991-1994 kabla ya kwenda kidato cha tano na sita katika Taasisi ya Biashara Shinyanga (SHYCOM) akisoma masomo ya Biashara hii ilkuwa ni Mwaka 1995-1997.
Safari ya elimu ya juu Kijaji alinza katika chuo kikuu Mzumbe akibobea katika uchumi alisoma tangu Mwaka 1998-2001 na kutunukiwa shahada ya juu yaani (Advanced diploma) ya Mipango ya Uchumi ;Stashada hiyo ya juu ni sawa na shahada ya sayansi katika uchumi ambayo inatolewa na chuo kikuu cha Mzumbe hivi sasa.
Mara baada ya kuhitimu stashahada hiyo alipata fursa ya kuendelea na masomo ya juu nchini Norway katika chuo kikuu cha Kristiansand alifanya masomo yake chuoni hapo tangu Mwaka 2006-2008 na kutunukiwa shahada ya umahiri ya sayansi (MSc) katika usimamizi wa Biashara akajikita zaidi kwenye usimamizi wa kimataifa,lakini pia kati ya Mwaka 2008 hadi 2013 Dk Kijaji alifanya kazi kama mtafiti mwandamizi katika chuo kikuu cha Agder akiwasaidia Maprofesa katika ufundishaji na utafiti.
Mwaka 2009 hadi 2014 Dk kijaji alifanya kazi kama mhadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe katika mafunzo ya ushauri wa kitaalamu na ustawi hasa katika utengenezaji na uchambuzi wa Sera, Uchambuzi wa Kitaasisi, Uchumi wa kazi na Maendeleo, Usimamizi wa Kistratejia,Maendeleo ya vijijini, Usimamizi wa miradi na masuala ya ushirika wa kimataifa kwenye masuala ya uchumi.
July 2014 kukaribia uchaguzi Mkuu alikuwa Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Mzumbe akifundisha masomo ya uchumi na baadae kuingia katika ulingo wa siasa ambapo alichukua fomu Mwaka 2015 na kugombea ubunge katika jimbo la Kondoa vijijini Mkoani Dodoma na kupata nafasi hiyo kuwakilisha wana kondoa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha katika serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya Hayati Dk John Joseph Pombe Magufuli alipata nafasi ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na kuwa katika Baraza la Mawaziri kama Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi ambapo katika nafasi hiyo akiwa kama Waziri amehudumu kwa muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya tano na mnamo Sept 12, 2021 Dk Kijaji kwa mara nyingine ameteuliwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania hii inadhihirisha ni namna gani wanawake wanaweza kushika nyazifa kubwa nchini Tanzania.
Kazi iendelee.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa