Na. Lina Sanga
Katika kuadhimisha miaka miwili ya Mbunge wa jimbo la Makambako ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe,Mhe. Deo Sanga imeelezwa kuwa amechangia zaidi ya shilingi milioni 426 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za kijamii ndani na nje ya jimbo la Makambako.
Hayo yamebainishwa katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2020-2025 , kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia julai 2020/2021 hadi februari 2022/2023,uliofanyika leo katika ukumbi wa greeb city Makambako.
Mhe. Sanga amesema kuwa fedha hizo anazotoa katika kuchangia maendeleo ni fedha ambazo huzitoa ngazi ya Kata,Mtaa na Kijiji baada ya kupokea maombi yao na fedha zingine ni gharama za shule za watoto wenye uhitaji,taasisi za dini na mwananchi mmoja mmoja ambao hufika nyumbani kwake kuomba msaada.
Amewataka wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na madiwani ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Makambako ,Kenneth Haule amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili, Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi bilioni 63.4 ambapo bilioni 1 zimeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na zingine kwa ajili ya malipo ya mishahara ya watumishi na matumizi mengine.
Wakati huo huo,Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Njombe amempongeza Mbunge wa jimbo la Makambako,kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa na kuchangia ujenzi wa vituo vya afya.
Ametoa rai kwa wananchi kuthamini uwepo wa mbunge huyo,kwani mambo anayoyafanya katika jimbo lake ni tofauti na Wabunge wengine.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe,Mhe. Justine Nusulupila Sanga ametoa rai kwa Serikali kuwapa haki ya umiliki wa miradi viongozi wa chama kuanzia ngazi ya tawi ili waweze kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa