Na. Lina Sanga
Njombe
Wito huo umetolewa na William Sapula,Mwanafunzi wa chuo cha Mgao training institute kilichopo Mkoani Njombe,katika kongamano la kujadili maendeleo endelevu ya Wilaya ya Njombe na Taifa kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika desemba 9,2022 ukumbi wa Njombe Sekondari.
William amebainisha kuwa,kutokana na vijana kutokombolewa kifikra wanazidi kuchanganyikiwa na kuishia kufanya mambo yaliyo nje ya maadili ya Kitanzania,hali inayoashiria kutoweka kwa Uhuru uliopo kutokana na kukosekana kwa ukombozi wa kifikra kwa vijana kuanzia ngazi ya familia na taifa.
“Kukosekana kwa ukombozi wa fikra za vijana ni sababu kuu ya vijana kukosa maadili ikiwa ni pamoja na uvaaji wa mavazi yasiyo na maadili,na wazazi na Serikali hawana muda wa kuweka mikakati ya ukombozi wa fikra za vijana mwisho wa siku vijana wanajikita sana kwenye fasheni za maisha na sio kutafakari Uhuru uliopiganiwa miaka 61 iliyopita na kuweka mikakati ya kimaisha kuendana na maadhimisho haya ya Uhuru wa nchi yetu hali inayosababisha,vijana kukosa uzalendo kwa taifa lao kwa sababu wamechanganyikiwa kiakili na wamepoteza muelekeo”,alisem William.
Ametoa wito kwa wazazi,walezi na Serikali kuweka mikakati ya kubadili na kuzikomboa fikra za vijana nchini,ili kuendana na miaka 61 ya Uhuru na sio kuweka mikakati katika maboresho ya miundombinu pekee.
Bi. Judica Omari,Katibu Tawala Mkoa ametoa pongezi kwa washiriki wa kongamano hilo la kujadili maendeleo endelevu ya Wilaya ya Njombe na taifa kwa ujumla,na kuahidi kufanyia kazi suala la ukombozi wa fikra za vijana ili kuendana na miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Aidha,ametoa shukurani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongezwa na Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kutoa fedha za ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu shule ya Msingi Idofi,iliyopo katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Jumla ya Mil. 960 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru kwa mwaka huu,Serikali iliagiza zitumike kwa ujenzi wa mabweni ya watoto wenye mahitaji maalumu katika Mikoa tisa ikiwamo Mkoa wa Njombe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa