Na. Lina Sanga
Njombe
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya hafla ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ludewa,Mhe. Victoria Mwanziva na kuwataka viongozi wote kusimamia ajenda za maendeleo kwenye maeneo yao.
Mhe. Mtaka amesema kuwa, ipo haja ya viongozi kuwa na ajenda za maendeleo ya maeneo yao ya utawala na wananchi watambue misimamo yao katika utoaji wa maamuzi sahihi kwa manufaa ya wananchi wanaongoza.
Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote kuitisha vikao vya wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni sambamba na kufanya ziara kila Kata kwa lengo la kukutana na wanufaika wa mikopo ili kutambua idadi ya vikundi vilivyopata mikopo kwa kila Kata.
Pia, ametoa rai kwa Madiwani wote kusimamia maendeleo ya wapiga kura wao na kutokuwa wapinzani kwa Wakurugenzi,katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Halmashauri na wananchi wao.
Ametoa rai kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe, Mhe. Deo Sanga kuhakiki maombi ya udiwani ,ili kupata watu wenye lengo la kutumia udiwani kufanya maendeleo kwa ajili ya wananchi na sio wao binafsi.
Ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhakikisha wanaleta matokeo,kwa kubuni vyanzo vya mapato ili kuongeza makusanyo ya Halmashauri.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa