Na. Lina Sanga
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Mabalozi wa nyumba kumi wametakiwa kutekeleza zoezi la Sensa kwa uzalendo,kwa kutambua Sensa ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe,Sure Mwasunguti katika mkutano wa mwisho uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya sekondari Makambako, wa kuhamasisha ushiriki wa Sensa ya watu na makazi itayoanza agosti 23 hadi agosti 31,2022.
Mwasunguti amesema kuwa,utekelezaji wa zoezi la Sensa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi,Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan ndiye msimamizi mkuu wa Sensa hivyo kila mwana chama wa CCM hana budi kuhakikisha anashiriki kikamilifu na malengo ya Serikali yatimie.
Ameongeza kuwa,kutokana na umuhimu wa Sensa kila balozi ajitoe kushiriki zoezi hilo kiukamilifu na kuhakikisha linafanikiwa kwa uzalendo mkubwa,ili ilani ya chama iendelee mbele.
Pia ametoa wito kwa Wenyeviti wa Mitaa kuwashirikisha mabalozi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao ya kazi,kwani mabalozi wana umuhimu mkubwa katika jamii hadi ndani ya chama na kuwaagiza
#Jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa