Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa na Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji Makambako,Kassim Mamba katika Mafunzo ya kabla ya Mkopo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Makambako leo.
Bw. Kassim amesema kuwa, baadhi ya viongozi wa vikundi wamekuwa na tabia ya kutowajulisha wana kikundi wengine kuhusu fedha ya mkopo waliyoomba kuingizwa kwenye akaunti ya kikundi, na kudiriki kugawana mikopo hiyo wenyewe na kuibua malalamiko kwa wana kikundi dhidi ya Halmashauri kutowapatia mkopo.
Amesema kuwa, ipo haja ya viongozi kujitahidi kuwa waaminifu kwa wanavikundi wote, ili kila mmoja anufaike na mkopo kama maombi yalivyowasilishwa na kuhakikisha marejesho yanafanyika kwa wakati ili vikundi vingine vinufaike pia.
Awali akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Bi. Appia Mayemba amewataka wanufaika wote wa mikopo kutumia fedha hizo kufanikisha malengo waliyokusudia ili waweze kupata faida na kurejesha mikopo kwa wakati badala ya kutumia katika vitu ambavyo haviwezi kuzalisha chochote.
Katika mafunzo hayo wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 wamepata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kilimo,ufugaji,lishe,afya,biashara,viwanda na uwekezaji pamoja na elimu ya fedha iliyowasilishwa na afisa mauzo wa benki ya NMB,Winfrida Mghamba.
Jumla ya Mil. 76 zimetolewa wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 , ambapo jumla ya vikundi vya Wanawake 9, Vijana 3 na watu wenye ulemavu 8 wamepata mikopo katika kipindi cha robo ya pili katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa