Na. Lina Sanga
Dodoma
Waajiriwa wapya wa kada ya ualimu na afya wametakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kabla au ifikapo juni 11, Mwaka huu vinginevyo nafasi hizo watapewa wengine wenye sifa.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaki za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) katika kikao kazi cha Maafisa habari wa Mikoa,Halmashauri na taasisi zilizopo Chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI kilichofanyika leo Jijini Dodoma,katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Bashungwa amesema kuwa waajiriwa wapya wa kada ya ualimu waliopata ajira ni asilimia kumi tu,na asilimia tisini ya waombaji wamekosa nafasi hizo,kibinadamu inauma lakini wasikate tamaa ajira zitaendelea kutangazwa
"Nitoe wito kwa waliokosa ajira wasikate tamaa waendelee kuvuta subira ajira zitaendelea kutangazwa,kazi ya kugawa riziki ni ngumu sana ajira zilipotoka tulisimamia vigezo na masharti lakini kwa sasa kuna memes zinazunguka nimekua mzee kabisa lakini tumetenda haki yeyote anayetaka kukagua utaratibu uliofanyika aje kila kitu kipo",alisema Bashungwa.
Pia,amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kuripoti shuleni ifikapo julai 4, vinginevyo nafasi zao watapangiwa wanafunzi wa akiba.
Ametoa wito kwa wazazi wa wanafunzi hao kuhakikisha watoto wanaripoti shuleni ndani ya muda uliopangwa,na kuanza masomo kwani wanafunzi wenye uhitaji wa nafasi hizo ni wengi.
Aidha,amewataka walimu wakuu na wakuu wa shule kutotoza michango yoyote nje ya nyaraka na miongozo ya Serikali,na hatua stahiki zitachukuliwa kwa mwalimu atayekiuka maagizo hayo.
Ametoa Wito kwa Makatibu wa wizara, wakuu wa Mikoa, wakurugenzi na Maafisa elimu kusimamia ipasavyo suala la michango shuleni ili kuondoa sintofahamu inayoweza sababishwa na baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakuu kutozingatia miongozo na nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
Jumla ya waajiriwa wapya wa kada ya Ualimu ni 9,800 na kada ya afya 6,876 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na jumla ya nafasi 736 za kada ya afya zitatangazwa tena baada ya Kukosa waombaji wenye sifa .
Kada hizo ni madaktari wa meno,teknolojia ya mionzi,tabibu msaidizi na tabibu wa meno.
#jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa