Na. Lina Sanga
Wito umetolewa kwa wadau wa elimu wenye uwezo wa kuanzisha vituo vya kutolea elimu kwa watoto waliokosa elimu,katika mfumo rasmi MEMKWA kwani idadi ya wahitaji wa elimu hiyo na vituo vilivyopo havitoshelezi.
Wito huo umetolewa leo na Kaimu mthibiti ubora Halmashauri ya Mji Makambako Vitalis Genda, katika maadhimisho ya wiki la elimu ya watu wazima yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Kahawa.
Genda amesema kuwa elimu ya MEMKWA ni muhimu sana kwani inapunguza idadi ya watoto na watu wazima wasiojua kusoma na kuandika,hivyo kwa wadau wa elimu wenye uwezo wa kuanzisha vituo hivyo waanzishe ili kushirikiana na Serikali kupunguza idadi ya watu wasiojua Kusoma na kuandika nchini.
Aidha,amewataka watu wazima wasiojua kusoma na kuandika kujitokeza na kujiunga mafunzo ya MEMKWA,kwani elimu hiyo ina manufaa makubwa kwa maendeleo yao.
Katika maadhimisho hayo zana mbalimbali za kufundishia na kujifunzia watoto wenye mahitaji Maalumu,zilionyeshwa kama zana za kujifunzia watoto wenye uoni hafifu na wasio ona kabisa,viziwi na watoto wenye ulemavu lakini pia maonyesho mbalimbali ya watoto hao yalionyesha kudhihirisha mafanikio ya elimu jumuishi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa