Ni Picha ya pamoja katika zoezi la kupokea Mifuko ya Cement takribani Arobaini,iliyotolewa na Umoja wa Vikundi vinavyolea watoto wadogo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako (UWAVIKUWAMA),
Zoezi hilo limefanyika katika Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo na Rasmi katika zoezi hilo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Ndg Hanana Mfikwa ambapo amesema Makambako itajengwa na wana Makambako wenyewe " Ni jambo zuri na jema kujitoa kwaajili ya Halmashauri yetu kwani uwepo wa vituo hivi umetoa Ajira kwa vijana wengi katika Halmashauri yetu na pia inaongeza uchumi kwa waajiriwa lakini uwepo wa vituo hivi unasaidia kupunguza masuala ya ukatili Majumbani hasa kwa wazazi ambao hawana wasaidizi wa karibu kwa watoto wao.
Mifuko hiyo imetolewa na kuelekezwa kufanya kazi katika Shule shikizi Maguvani kata ya Maguvani ,Shule ya Msingi kwauchungu ,Shule Shikizi ya Mfumbi na Shule ya Msingi Maendeleo ,aidha Matumizi ya Mifuko hiyo ni pamoja na kusaidia Ujenzi wa Madarasa ,ofisi za walimu na ujenzi wa matundu ya vyooo.
Katika Risala umoja huo wameeleza lengo lao kujitoa hasa katika Maendeleo ya Elimu kwa watoto wadogo Halmashauri ya Mji wa Makambako na kuwasaidia Wazazi wa Makambako katika kupiga vita suala la ukatili kwa watoto wajumbani kwani Umoja huo kwa sasa unawatoto takribani zaidi ya 2000 kwa Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Naye afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Mji wa Makambako Bwana Regis Ng'itu kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii amesema kuwa wamejipanga vizuri kufanya kazi na Umoja huo hasa kwa kufuata sheria za Nchi katika masuala mazima ya ulinzi na usalama wa watoto kwa kufuata taratibu husikaAkihitimisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya ,Mji wa Makambako Paulo Malala, Amesema kuwa zoezi hilo ni jema kwani kutoa cement mifuko takribani Arobaini tayari wamechangia sekta ya Elimu hivyo kama kuna wadau wengine wenye nia njema na Halmashauri ya Mji wa Makambako wajitokeze kwani tupo kwaajili ya kazi na Maendeleo ya Tanzania na amewashukuru kwa Kujitoa kwao na kuahidi mifuko hiyo itafika mahala husika kwa kazi husika na kwa wakati husika.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa