Na. Lina Sanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako na Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara ,wametakiwa kuhakikisha wafanyabiashara wa mazao na mali mbichi wanafanyia biashara zao katika maeneo yaliyoainishwa kulingana na aina ya biashara zao.
Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa katika Mkutano wa baraza la Madiwani la kuishia kipindi cha robo ya tatu(Januari – Machi) 2022/2023,uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Mhe. Hanana amesema kuwa,Halmashauri haitatoa muda wa nyongeza tena kwa wafanyabiashara wa mazao ambao walianza ujenzi wa maghala, katika Mtaa wa Kiumba kwani muda wa nyongeza uliotolewa katika mikataba ya ujenzi wa maghala hayo unaisha Juni 30,2023 na kuwataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanakamilisha ujenzi ndani ya muda uliopangwa ili maghala hayo yaanze kutumika ifikapo Julai 1,mwaka huu.
Pia,amewataka wamiliki wa nyumba zinazotumika kama stoo za mazao kuzingatia barua za zuio la nyumba za makazi kutumika kama stoo za mazao,kwani madawa yanayotumika kuhifadhia mazao yana athari kubwa kwa wakazi wa nyumba hizo hususani watoto.
“Hatukatai mtu yeyote kufanya biashara mahali popote bali tumekataa kuweka maghala kwenye nyumba za kuishi watu,mtu yeyote ambaye hana mahali pakufanyia biashara amuone Mkurugenzi amuonyeshe mahali pakufanyia biashara ambapo ni rasmi kwa ajili ya biashara”,alisema Mhe. Hanana.
Aidha,ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mali mbichi katika soko kuu la Makambako kushusha na kuuza bidhaa zao ,katika masoko yaliyoainishwa na Halmashauri ili kuendelea kuupanga mji kuanzia.
Mnamo Mei 25,mwaka huu Halmashauri ya Mji Makambako ilitoa tangazo la mwisho kuwataka wafanyabiashara wa mali mbichi,kuanza kushushia bidhaa kwenye masoko ya Magegele na Maguvani na mwisho wa kushusha bidhaa hizo soko kuu ilikuwa ni Mei 29,2023.
Magari yote yanayoleta ndizi na matunda yanatakiwa kushusha bidhaa hizo katika Soko la Maguvani na Viazi katika Soko la Magegele, na Mfanyabiashara hazuiliwi kuuza bidhaa zake katika masoko hayo au soko kuu.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa