Na. Lina Sanga
Njombe
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maji,Mhe. Jumaa Aweso alipokuwa akitoa salamu kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo Mkoani Njombe.
Mhe. Aweso amesema kuwa huduma ya maji sio biashara bali ni huduma,hivyo Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji watoe Maji kwa maana ya huduma na sio kuwabambikizia wananchi bili za maji,kwani maji ni usalama wa taifa ukiwa na maji toshelezi uhakika wa usalama wa chakula,nishati na usalama wa ndoa unakuwepo,Wizara ya Maji itahakikisha usalama wa ndoa za kina Mama.
Mhe. Aweso amesema kuwa miaka ya nyuma Serikali iliwekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa Miradi ya Maji lakini matokeo hakuna na ilionekana ni kawaida,lakini pia wananchi wanaoishi vijijini kukosa maji na kunywa maji pamoja na mifugo ilionekana ni kawaida,lakini sasa miradi mikubwa ya maji imejengwa hadi vijijini na Wizara ya Maji iliyokuwa ni Wizara ya Kero na lawama hivi sasa imekuwa Wizara ya utatuzi.
Ameongeza kuwa Wizara ya maji haijaajiri vibaka kutekeleza miradi ya maji,bali imeajiri wataalamu ili kuhakikisha watanzania wote wanapata maji safi na salama.
"Mhe. Rais tukuhakikishie Wizara Ya Maji haijaajiri vibaka,Wizara imeajiri wataalamu tutahakikisha watanzania wanaoishi Mijijini na Vijijini wanapata maji safi na salama",alisema Mhe. Aweso.
Pia,amesema kuwa moja ya changamoto kubwa ni miradi kichefuchefu katika taifa, ambapo jumla ya miradi 177 iliainishwa na baada ya kuanzishwa kwa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) jumla ya miradi 130 imeshakwamuliwa hadi kufikia mwezi disemba miradi yote itakamilishwa.
Mhe. Aweso amesema kuwa Wizara ya Maji imejipanga vizuri kuendelea kuwatua kina mama ndoo kichwani kwa kujenga miradi mikubwa ya Maji Njombe Mjini,Makambako na Wanging'ombe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa