Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe. Anthony Mtaka katika kikao cha uzinduzi wa mwongozo wa elimu Mkoa wa Njombe kilichofanyika leo shule ya Msingi Mpechi.
Mhe.Mtaka amesema kuwa walimu wengi wamekuwa na kawaida ya kutoa visingizio vya kiafya na masuala ya kifamilia ili wapewe uhamisho,hivyo kabla ya kuanza kuwasumbua Maafisa elimu na Utumishi juu ya uhamisho mtumishi hana budi kuchagua kazi au sababu ya kuomba uhamisho.
"Kuna ajira mpya wametuma maombi ya kazi zaidi ya mara tatu na kukosa,lakini baada ya kupata kazi anaanza kiguu na njia kutaka abadilishiwe kituo cha kazi au ahamishwe anasahau maombi aliyokuwa anaomba na wengine hadi waliokoka,Mungu kawasaidia kupata kazi anaanza kusumbua",alisema Mhe. Mtaka.
Amewaagiza maafisa elimu wote katika Mkoa wa Njombe kutopitisha barua zinazohusu uhamisho wa walimu wala kupokea simu za watu juu ya uhamisho wa walimu taarifa zifikishwe kwa Mkuu wa Mkoa na sio Katibu Tawala Mkoa.
"Mimi huwa sifanyi kazi na kimemo kama una ndugu unategemea atapiga simu ili ubadilishiwe kituo cha kazi,hakuna mtu atayekubadilishia kituo na sio kazi ya afisa elimu,simu yoyote afisa elimu ukipigiwa usimwambie Katibu Tawala Mkoa waambie mpigieni Mkuu wa Mkoa,ameweka zuio na hakuna mwalimu aliyekuja Njombe kwenye ajira mpya atayebadilishiwa kituo wala kuhama"alisema Mhe. Mtaka.
Ametoa wito kwa watumishi wapya kutunza kazi waliyopata, wachezee mshahara na sio kazi lakini pia kumshukuru Mungu kwa kupata ajira kwani kuna maelfu ya vijana wenye digrii waliomba nafasi hizo wamekosa.
Pia amesisitiza nidhamu katika maeneo ya kazi kwa walimu wapya kuwaheshimu na kuwasikiliza walimu waliowakuta shuleni,pamoja na kujifunza na kuachana na kiburi cha digrii walizonazo,kujiepusha na masuala ya utoro na ulevi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa