Na. Lina Sanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Kenneth Haule akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi,mabalozi kutoka mitaa yote,Watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Mji Makambako kuhusu ushiriki wa zoezi la Sensa.
Haule ametoa wito kwa viongozi wote waliohudhuria mkutano huo kutoa elimu ya umuhimu wa sensa kwa watu wote wa makambako kwani zoezi la sensa lina muda maalumu wa kuanza na kumalizika,hivyo kila mwananchi ahakikishe anahesabiwa ili zoezi likamilike kwa muda uliopangwa.
"Zoezi la Sensa linatakiwa kutolewa ripoti ya utekelezaji kila siku ,hivyo sitarajii Makambako kushika nafasi ya mwisho katika zoezi hili la Sensa tusaidiane kuwapa elimu wengine juu ya umuhimu wa Sensa na kuifanya Makambako yetu iwe mfano kwa kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi na ndani ya muda uliopangwa",amesema Haule.
Sensa ya watu na Makazi inaanza rasmi usiku wa kuamkia tarehe 23 agosti hadi agosti 31,2022 na kesho agosti 21 na 22 zoezi la Sensa litaanza rasmi kwa kujaza dodoso la huduma za jamii na ukaguzi wa mipaka.
#jiandaekuhesabiwa2022
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa