Na. Lina Sanga
Njombe
Tamko hilo limetolewa leo na Waziri wa Uwekezaji,Biashara na Viwanda, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika mkutano wa saba wa baraza la biashara, Mkoa wa Njombe lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe , na kuwakutanisha wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Njombe ili kusikiliza na kujadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Mhe. Kijaji amesema kuwa Wananchi hao ambao hawakufanyiwa uthamini wa maeneo yao wakati wa uthaminishaji wa awali na kushindwa kulipwa fidia ya maeneo yao , Wizara imeanza kufanyia kazi suala hilo ili kumalizana na wananchi hao , ili pindi wadau wa kujenga soko hilo watakapo patikana ujenzi uanze mara moja bila kikwazo chochote.
Amesema kuwa endapo ujenzi wa soko hilo la Kimataifa na bandari kavu katika Halmashauri ya Mji Makambako ukikamilika,utasaidia kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa katika Mkoa wa Njombe na wananchi wataweza kunufaika na kujipatia maendeleo.
Ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya nchini kusimamia Sekta binafsi katika maeneo yao na kuzilea ili zikue na kutokuwa kikwazo katika ukuaji wa Sekta hizo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani Sekta binafsi ndizo zimebeba uchumi wa taifa.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa