Na. Lina Sanga
Njombe
Wito huo umetolewa na Afisa rasilimali watu Mwandamizi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi. Joyce Shala katika semina ya wadau wa bodi hiyo, Katika Mkoa wa Njombe iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Shala, amesema kuwa tangu kufungwa kwa benki ya NJOCOBA (NJOMBE COMMUNITY BANK) januari,2018 ilikuwa na wateja 12,323 na waliolipwa fedha za fidia ya bima ya amana ni 4,014 sawa na asilimia 87, ambao bado hawajachukua ni wateja 8,309.
"Niwaombe wateja ambao bado hawajachukua fidia ya bima ya amana wafuate fedha hizo benki ya biashara ya Taifa (TCB), zamani ilitambulika kama benki ya posta,wakiwa na vitambulisho vya Taifa(NIDA),mpiga kura au hati ya kusafiria", alisema Bi. Shala.
Naye, Adv. Acley Chaula, Afisa sheria mwandamizi wa bodi ya bima ya Amana (DIB) amewataka wadaiwa wote wa benki ya NJOCOBA,kulipa madeni yao ili fedha hizo zirejeshwe kwa wateja wa NJOCOBA,vikundi na kumaliza madai ya wenye hisa na wadai wengine.
Amewataka wadaiwa wote kurejesha fedha wanazodaiwa kabla ya maamuzi ya kuuza mali zao hayajafanyika, kwani kufungwa kwa benki sio kufutwa kwa deni.
Jumla ya watu 200 wanadaiwa na benki ya NJOCOBA kiasi cha shilingi mil. 400 tangu benki hiyo ifungwe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa