Na. Lina Sanga
Kenneth Haule,Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Mji Makambako ametoa rai kwa wasimamizi wa vituo vya uchaguzi kuwa mabalozi wa amani kuelekea siku ya uchaguzi,ili amani itawale hata baada ya uchaguzi.
Haule ametoa rai hiyo leo katika ufunguzi wa semina ya mafunzo elekezi kwa wasimamizi hao,iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Makambako na kuwataka kutumia busara na hekima kusuluhisha migogoro katika siku za kampeni na siku ya kupiga kura.
“Tunataka baada ya novemba 27 Makambako iendelee kufanya shughuli zake za kawaida kama hakukuwa na uchaguzi,amani itawale kwa sababu wanaosimamia uchaguzi,tunaosema viongozi wa vyama vya siasa, wagombea na watendaji wa Serikali wote tunaishi Makambako moja,itakuwa jambo la ajabu sana uchaguzi utusambaratishe”,alisema Haule.
Aidha, amewataka wasimamizi hao kusimamia uchaguzi kwa mujibu wa taratibu watakazo elekezwa na wasimamizi ngazi ya Halmashauri, na kuwakumbusha wagombea na mawakala wa vyama vya siasa kuwa matokeo ya uchaguzi ni matatu,kuna kushinda,kushindwa na kutoka droo hivyo hawana budi kuyapokea ili baada ya uchaguzi shughuli za kawaida ziendelee.
Mwl.Veronica Malifimbo na Mwl. Timothy Msigwa kwa niaba ya wasimamizi wa vituo vya uchaguzi wamekiri kutunza viapo vya utii kuelekea siku ya uchaguzi, na kutoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura ili waweze kuchagua viongozi watakao waongoza kwa kipindi husika.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa