Na. Lina Sanga
Wito huo umetolewa leo na Meja Daniel Shija Mawenge,Kaimu Kamanda Kikosi cha Jeshi la Wananchi 514KJ,alipokuwa akihutubia wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako waliofika kufanya usafi katika Kituo cha afya Makambako,ikiwa ni utekelezaji wa shughuli za kijamii katika wiki la Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika.
Meja Daniel amesema kuwa,Tanganyika ilipata Uhuru Mwaka 1961 kwa amani bila umwagaji damu,hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuilinda amani ya nchi na kudumisha umoja ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu.
“Tanganyika ilipata uhuru bila kumwaga damu kutoka kwa wakoloni mataifa mengi yamepata uhuru kwa kumwaga damu,ndio maana hata bendera zao zina rangi nyekundu lakini bendera yetu haina rangi nyekundu, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kudumisha amani na umoja kwenye makazi yake yanayomzunguka kwa maslahi mapana ya taifa letu”,alisema Meja Daniel.
Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru kwa mwaka huu yanafanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na upandaji miti,michezo,usafi wa mazingira,mashindano ya michezo na sanaa,mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na kufanya kongamano na mdahalo wa kujadili maendeleo endelevu ambayo Wilaya,Halmashauri na Mkoa imefikia kwa kipindi cha miaka 61 ya Uhuru.
Katika Halmashauri ya Mji Makambako Mdahalo wa kujadili maendeleo endelevu ya Halmashauri utafanyika desemba 8,2022 ,katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Makambako, ukihusisha watumishi wa Serikali na taasisi zote zilizopo katika Hlmashauri ya Mji Makambako,wazee wa mji na wananchi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru kwa mwaka 2022 inasema"Amani na Umoja ni nguzo ya maendeleo endelevu".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa