Na. Lina Sanga
Mhe. Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya leo ameridhia pendekezo la Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka la kiwanda cha mipira ya mikono (MSD ) Idofi,katika Halmashauri ya Mji Makambako kuzalisha mipira ya kiume(Kondomu) kwani mali ghafi za uzalishaji zinaendana na mipira ya mikono inayozalishwa kiwandani hapo.
Akiridhia pendekezo hilo,Mhe. Ummy amesema kuwa endapo bidhaa hiyo itazalishwa katika kiwanda hicho , itasaidia kupunguza gharama ya ununuzi wa bidhaa hiyo nje ya nchi ambapo kwa sasa jumla Mil. 10 zinatumika kununua kondomu.
Amesema kwa sasa wanachotaka ni watu kuendelea kutumia kinga kwani UKIMWI na magonjwa ya zinaa bado yapo na kutokana na umuhimu wa bidhaa hiyo ni vema zitengenezwe ndani ya nchi na zitengenezwa katika kiwanda cha mipira ya mikono Idofi, katika Halmashauri ya Mji Makambako,Mkoani wa Njombe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa