Ni ziara ya Mh Mbunge wa jimbo la Makambako, Deo Sanga katika vijiji vitatu vya Halmashauri ya Mji wa Makambako ,vijiji hivyo ni pamoja na Kijiji cha Mawande ,Utengule na Ikelu.Katika ziara hiyo Mbunge Deo Sanga ameongozana na wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa lengo la kujibu maswali ambayo wananchi watahitaji ufafanuzi juu ya miradi inayoendelea katika maeneo yao hususani miundo mbinu ya Barabara ,Umeme ,Maji ,Afya, Elimu na mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye mahitaji maalumu.
Lengo la ziara ya Mbunge katika vijiji hivyo ni pamoja na kutembela na kuona maendeleo ya miradi pangwa ambayo serikali imetoa fedha kwaajili ya wananchi na kuona fedha ambavyo zinafanya kazi, kusikiliza kero za wananchi ambazo zitajiiwa na wataalamu wa Halmashauri kwa ufafanuzi zaidi,kutoa mrejesho wa bajeti ya mwaka 2021/2022 na kuona maendeleo ya fedha ambazo amekuwa akitoa kama mchango wake katika maendeleo, Je zinafanyiwa kazi vizuri hasa katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa vijiji hivyo..Aidha Katika ziara hiyo mbunge amapokea tarifa ya maandeleo ya vijiji hivyo hasa kwa kuorodhesha michango mbalimbali iliyotolewa na mbunge, Serikali na nguvu za wananchi kwa kuanza na kijiji cha:
Utengule :Jumla ya fedha ni shilingi 26704000 kwa kuanza mwaka 2015 mpaka sasa fedha hizo zimetumika katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi katika kanisa la kilutheri ,vifaa vya michezo usafirishaji wa trip za mchanga katika ujenzi na ukatabati wa shule ya msingi Utengule ,Nyumba ya mwalimu Ununuzi wa mbao ,mifuko ya saruji ,ulipaji mafundi katika ujenzi wa zahanati ,mbao misumari ,Gegi thelathini,,kenchi ,Bati na koa ,na kuchangia fedha kwaajili ya kuingiza umeme katika shule ya msingi lungwa kwa ofisi moja madarasa mawili na nyumba nane za walimu katika shule hiyo.
Kijiji cha Mawande kwa kipindi cha miaka mitano Mbunge Deo sanga ametoa kiasi cha shilingi 5130000 (Milion tano laki moja na elfu thelathini ambazo zimetumika katika ujenzi wa vyoo shule ya msingi Mawande ,vifaa vya michezo ,upauaji wa nyumba ya mwalimu ,utengenezaji madawati ,ukarabati wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mawande pamoja nakutoa gari la kusaidia ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Mawande.
katika kiji cha ikelu vile vile mchango wake mkubwa katika miradi ya maendeleao hususani vifaa vya michezo kwa vijana na shule ya msingi ikelu na nyambogo aidha katika upande wa afya mbali na kuwa kwa sasa tayari wananchi wameanza kujenga kituo cha afya ,lakini pia ametoa sinki moja la choo kwaajili ya watoto wenye ulemavu shule ya msingi Ikelu na kuahidi kuwasaidia vijana kasa wanaojihusisha na masuala ujasiriamali pamoja na kutoa mifuko hamsini ya saruji kwaajili ya ujenzi wa shule shikizi katika kijiji hicho.
Kwa pamoja katika ziara hiyo kwa vijiji hivyo vitatu mbali na kutoa vitu vya maendeleao kwa idara ya Elimu, afya, vifaa vya michezo kwa vijana na tofali kwaajili ya mwendelezo wa ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Mawande amesisitiza suala la kudumisha upendo, amani na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa awamu ya sita Samiah Suluhu hassan na zaidi kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kuchukua tadhari juu ya janga la ungonjwa wa Corona.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa