Na. Lina Sanga
Timu ya Hamasa ya Tume huru ya Uchaguzi leo ipo katika Halmashauri ya Mji Makambako kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani 2025.
Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika Halmashauri ya Mji Makambako litaanza rasmi januari 12 hadi 18, 2025 katika Kata zote 12 kwenye vituo 89 katika Mitaa,Vijiji na Vitongoji vyote.
Wahusika wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni wapiga kura wapya ambao wamefikisha umri wa miaka 18 ambaye hakuwahi kujiandikisha kwenye daftari na ambaye atatimiza umri wa miaka 18 ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025,anayeboresha taarifa zake kama amehama makazi ya awali alipojiandikisha kama Mkoa na Kata ,ambaye taarifa zake zilikosewa wakati wa kujiandikisha na aliyepoteza kadi au kadi imeharibika na aliyepoteza sifa za kuwemo katika daftari la kudumu la wapiga kula mfano,mtu sliyefariki.
Sifa za kujiandikisha kuwa mpiga kura ni awe raia wa Tanzania, awe ametimiza umri wa miaka 18 na awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi au sheria nyingine zilizotungwa na Bunge.
Vituo vya kujiandikishia vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufunga saa 12:00 jioni siku zote za uandikishaji.
Kauli mbiu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2024 inasema "Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa